GET /api/v0.1/hansard/entries/1520133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520133,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520133/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu wa Spika. Ninaunga mkono Mswada huu. Katika Kifungu 24(2) cha Katiba yetu, fedha hizi zitasaidia katika mambo ya kimsingi kama maji, barabara, afya na umeme. Huduma hizi zitaweza kufikishwa katika sehemu ambazo zilikuwa zimesahaulika na kuwachwa nyuma kimaendelo haswa kwa mambo ya maji, barabara, na afya. Tukiangalia haswa, tunaona zile kaunti kumi na nne ambazo ziifaa kusaidika na hazina hii ni kama Turkana. Ni maskitiko makubwa sana jamani tukiangalia shida za miundo msingi kama barabara, ukosefu wa maji, afya na ukame kule Turkana. Sehemu ya Lamu, Mandera, Wajir, sehemu nyingine za Kwale na sehemu nyingine za Kilifi na Marsabit pia ni maskitiko makubwa. Kama Wakenya, tunakubali kulikuwa na dhuluma na kutengwa kihistoria. Hii ni kwa sababu Serikali ilikuwa ni moja, Serikali kuu peke yake. Kila kitu kilikuwa kinapangwa kule juu, na kinamalizika kule juu. Kwa hivyo, sehemu nyingi zilikuwa zinasahaulika. Tushukuru sana kwa sababu hivi sasa kuna ugatuzi na tunaona maendeleo mengine kupitia njia ya ugatuzi. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu pia unapendekeza kuongeza maisha ya hazina hii. Ilikuwa ifike mwaka wa elfu mblili na thelathini lakini sasa, itaongezwa miaka kumi mingine zaidi. Hii ni kwa sababu bado tunaona sehemu ambazo zilitengwa ama zilidhulumiwa bado hawajafikia ile shabaha kwa mambo ya maji, barabara, umeme na hata kielimu. Hazijafika sehemu kama hizo. Kwa hivyo, ningependa kusema hata miaka kumi ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}