GET /api/v0.1/hansard/entries/1520134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520134,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520134/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "michache. Tuongeze ikue kama miaka ishirini. Miaka ishirini itakuwa miaka mizuri sana hivi sasa kwa sababu Rais William Samoei Ruto yuko imara kuhakikisha hizi fedha zitatumika kwa njia inayofaa na zitabadilisha maisha ya Mkenya, haswa yule ambaye ametengwa kwa miaka mingi. Pia, ni lazima tuwe na muundo msingi na taratibu muafaka za kuonyesha kutakuwa na usawa, kutakuwa na uwazi kwa kusambaza fedha hizi katika zile sehemu zilizotajwa. Kusiwe ya sehemu nyingine wanapata zaidi na nyingine wanapata chache. Pia, wananchi wenyewe waweze kuhusishwa vilivyo ili waseme shida ambazo zinakwaza sana katika mipango ya maji, barabara, afya na umeme. Kwa mfano, mnaeza amua kujenga visima sehemu fulani na kumbe visima havitatosha. Pengine sehemu hiyo wanahitaji mabwawa ili bali na kutumia maji nyumbani, wayatumie pia kwa kilimo. Tunastahili kuangazia pesa hizi kwa njia inayofaa na tutoe ufisadi. Dadangu Ruweida alizungumzia barabara ya Mtangawanda iliyotengenezwa kutumia pesa nyingi, na kulikuwa na wafadhili wengine, na inaonekana pesa zingine zilipotea. Ninamshukuru sana Rais kwa sababu juzi, Mhe. Ruweida, basi la kwanza lilibebwa na boti likafika kule Amu. Na hiyo yote ni mipango ya Rais William Samoei Ruto. Kwa hivyo, tunampatia kongole kwa jambo hilo. Tunataka Wakenya wawe sawa haswa katika mambo ya kimsingi ambayo yanatukwaza sana kama mambo ya maji. Kule Kwale na Kilifi kuna sehemu mpaka sasa kina mama wanachoka vichwa na migongo wakitembea kilomita nyingi sana kutafuta maji. Hatutaki kuona kuna kwingine katika Kenya ambapo maji iko kila mahali hata mpaka inatumika kiholela ila sehemu nyingine hakuna maji; sehemu nyingine kuna barabara zinaandikiwa mahindi, na sehemu nyingine watu hawajawahi kuona hata lami. Hawajui lami ni nini. Kuna jamii kama ya Wadorobo, jamii ya Ogiek ambazo hawajawahi kuona mambo mengi ya miundo misingi katika maisha yao. Mhe. Naibu Spika, tungependa pia turekebishe Mswada huu ili hata mambo ya elimu yaweze kushughulikiwa na fedha hizi. Kuna sehemu hawana national school na hawana hata"
}