GET /api/v0.1/hansard/entries/1520136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520136/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Yaani wako na shule za kiwango cha wilaya peke yake na hawana zile ambazo ziko katika hali ya shule zile nzuri kama Starehe Boys, kwa mfano. Kuna sehemu hawana shule kama hizo ambazo zinaweza kutoa watoto na natija juu sana ya kielimu. Kwa hivyo, ni lazima tuangalie mambo ya pesa hii na tuangalie nyanja nyingine ambazo hazijawekwa katika Katiba kuangaliwa na fedha hizi kama mambo ya chakula. Tumekuwa na ukame sana katika taifa letu. Sehemu za Tana River, Marsabit na sehemu zingine karne wamekuwa wakikosa chakula na wamekuwa na shida. Kina mama na watoto wanahangaika. Mifugo pia inakufa kwa sababu ya ukosefu wa maji, chakula na miundo misingi. Tumejua kuna ile board . Lazima iangaliwe, ipigwe msasa na iwe ni board ambayo itakuwa inafanya usawa haswa iweke vigezo na mikakati vile hizi fedha zitatumika. Sintofahamu ya Serikali kuu na serikali za kaunti pia lazima imalizike kwa sababu tunajua kaunti wanapata fedha zao. Ingekuwa muafaka kama Serikali kuu ingetumia mfumo wa hazina ya maendeleo wa maeneo bunge kwa pesa zile. Mbunge anaelewa matatizo nyeti katika mambo ya maji, barabara, afya na umeme. Anaelewa sana kuliko kaunti kwa sababu pengine kaunti ni kubwa sana. Fedha hizo zikipitishwa mashinani, hali ya maisha ya wakenya itabadilika. Mwaka huu wa elfu mbili ishirini na tano ni mwaka wa mageuzi kimaendeleo. Tukifanya Supplementary Budget, ni lazima tuweke pesa za kutosha kwa hazina hii kwa sababu ni kweli hatuko sawa katika sehemu zetu tunakotoka katika jamhuri ya Taifa letu la Kenya. Na hii yote ilitokana na ukabila wakati wa nyuma. Ndio maana tunaona Mhe. Rais kila saa anazungumzia ukenya ili tushikane tuwe Kenya moja na tuwe kitu kimoja. Ndio kila mkenya alipo apate maji, ana muundo wa msingi wa barabara na apate huduma kwa zahanati. Sasa hivi, maradhi ya saratani yameenea sana. Kina mama wengi wanakufa kutokana na ugonjwa saratani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}