GET /api/v0.1/hansard/entries/1520137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520137,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520137/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Je, sehemu ambazo zilitengwa na kusahaulika na sehemu nyingi kame, wana zahanati ambayo inaweza kuangalia saratani? Hilo ni swali lazima tujiulize. Kuna maradhi magumu mazito ambayo tuko nayo katika taifa letu la Kenya. Iwapo hatutakuwa na zahanati ambazo zina vifaa, madaktari, na madawa ya kutosha, basi wakenya wengi watapoteza maisha yao. Ndiposa tunasema, lazima tulipige jambo hili darubini. Pia tutakhimini taifa letu la Kenya, kaunti zetu arobaini na saba, maeneo bunge yetu mia mbili tisini, tujue ni sehemu gani ambazo zimetengwa, ziko nyuma na hazijapata maendeleo. Kwa hivyo, ninaunga mkono Mswada huu. Ninawaambia Wabunge wenzangu tuangalie mikakati ya sheria na mbinu na miundo misingi za kuonyesha vile fedha hizi zitamsaidia Mkenya ili Kenya ikue moja na Wakenya wote tufurahie."
}