GET /api/v0.1/hansard/entries/1520284/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520284,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520284/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Nimesikia kwa makini sana vile wenzangu wamechangia Mswada huu ambao umetoka Seneti. Mhe. Spika wa Muda, mwanzo ningetamani sana kulieleza Bunge hili la taifa kwamba walioandika Katiba walikusudia sana kufanya Kenya iwe sawa katika maendeleo ya nchi nzima. Wale walioketi na wakakubaliana na Wakenya wakapiga kura kwamba Katiba ipitishwe mwaka wa 2010, waliangalia sana Kipengele 204 katika Katiba yetu ya Kenya. Kinaleta wazo la kuwa na Equalisation Fund, ama mfuko wa kusawazisha. Hii ina maana kwamba Wakenya ambao walikuwa wamebaki nyuma kwa miaka mingi, ama sehemu za nchi zilizokuwa zimetengwa na central Government, ama Serikali ya kutoka Nairobi, ziweze kupata usawa. Hivyo, walileta Kipengele 204 katika Katiba yetu ya Kenya ili kusawazisha sehemu zilizobaki nyuma. Inatia wasiwasi sana kwamba Wakenya walipokubaliana hivyo… Shirika la CRA ndilo lililotwikwa mamlaka ya kutengeneza ile tunaita M arginalisation"
}