GET /api/v0.1/hansard/entries/1520286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520286/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": ", ili Article 204 iweze kufanyika kupitia hiyo M arginalisation Policy . Hii CRA iliamua na mara ya kwanza iliongozwa na yule aliyekuwa mkubwa wa Benki Kuu la Taifa, Bw. Micah Cheserem. Walikubaliana kwamba kaunti 14 za Kenya ziweze kutambulika kuwa zilibaki nyuma na ziweze kupewa pesa kupitia ile Article 204 ya Katiba. Hii ingeziwezesha kuinuka kimaendeleo kwa mfano katika afya, barabara, maji, na stima. Ni jambo la kutia uoga sana kwamba baada ya ile tume ya kwanza, ilipokuja tume ya pili, iliamua kwamba sehemu zilizobaki nyuma ziongezeke ziwe 34. Leo hii tunapoongea juu ya Mswada huu, tunaona maajabu. Nitakupa mfano wa Kaunti ya Taita Taveta. Ilikuwa kati ya zile 14 za mwanzo, zile Wakenya walisema zilibaki nyuma. Ingawa hivyo, CRA kwa kuwa na hekima ama kukosa hekima, wakaamua kwamba Taita Taveta iondolewe katika sehemu zile ambazo zilibaki nyuma. Kwa hivyo, tunapojadili huu Mswada leo, walitoa Taita Taveta. Nimeona wamerudisha kata ndogo mbili. Moja iko Voi na nyingine iko Taveta. Ati kata hizo ndogo ndizo zilizobaki nyuma! Wameacha kuhusisha sehemu zingine zote katika kaunti yetu ya Taita Taveta wakisema ziko sawa na zinaweza kulinganishwa na sehemu zingine. Hili ni jambo ambalo limeleta taharuki kubwa kule Taita Taveta. Kwamba leo hii,"
}