GET /api/v0.1/hansard/entries/1520291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520291,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520291/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": "katika hiyo Kaunti. Leo hii, ukitembea katika zile Kaunti 14, na kusikiliza wale ambao wameketi hapa wakilia, utagundua kuwa ni kwa sababu tuliachwa nyuma miaka hamsini baada ya uhuru. Ugatuzi ndio kidogo unatukumboa. Kama Bunge la Taifa, lazima tuambiane ukweli. Sehemu zilizobaki nyuma tunazijua. Tusije hapa tukajifanya kwamba Kaunti ya Kiambu imebaki nyuma na inapata pesa ya Equalisation Fund . Mbunge wa Homabay Town, ameshangaa kwamba kwake pia kuna sehemu imetajwa kuwa imebaki nyuma. Hata watu wanashangaa. Lazima tuambiane cha msingi na ukweli kwamba zile kaunti zinazojulikana zilibaki nyuma ni kama zile za north eastern, Pwani naTurkana. Kuna kaunti ambazo hata ukiuliza anyone in this country, they know where marginalisation has happened ."
}