GET /api/v0.1/hansard/entries/1520292/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520292,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520292/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "Namaliza kwa kusema hivi: Wenzangu Wabunge, jamani let us be honest . Tuwe watu wa ukweli. Kama sehemu moja katika kaunti yako imejumuishwa hapa na haipo katika zile kaunti 14 za mwanzo, ukipata hizo hela, basi unazidi kuleta marginalisation nchini Kenya. Hili ni suala nyeti sana. Kwa hivyo, naomba wale ambao wanaunga mkono huu Mswada, wasifanye hivyo kwa sababu kaunti yao imepata kitu ilhali haiukuwa miongoni mwa zile 14. Hii ni kwa sababu ukifanya hivyo, unadhalilisha Wakenya wengine katika maeneo mengine. Unafanya Mkenya mwingine akose huduma za afya ilhali huyo wa kwako anapata maradufu kwa sababu mmekuwa mkipata hizo hela tangu zamani. Mara nyingi, pesa za Kenya hufuata sehemu ambazo marais, mawaziri na wale mabwenyenye wanaosimamia Serikali wanatoka. Ndiyo maana Wakenya walikataa mfumo wa serikali moja na kupigia debe serikali ya ugatuzi. Kwa takriban miaka hamsini, kuanzia uhuru mpaka 2010, Kenya imekuwa ikisimamiwa na watu wachache; wale ambao wanasema ni wengi, wako na numbers na nguvu. Hao ndio wamekuwa wakinyanyasa nchi. Ndiyo sababu napinga huu Mswada. Nitauunga mkono wakati zile Kaunti 14 zilizokuwa mwanzoni zitakaporudishwa na kufaidi kutoka hizi pesa za Equalisation Fund ."
}