GET /api/v0.1/hansard/entries/1520326/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520326,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520326/?format=api",
    "text_counter": 317,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa na mimi nichangie Mswada ambao, tukiuangalia katika Kipengee cha Katiba 204(2), sehemu inayotakikana kuangaziwa zaidi ni mambo ya maji, miundo msingi, barabara, na vilevile umeme. Asante sana, Mhe. Farah Maalim, mzee wangu, mentor . Kwa hivyo, nashukuru sana, Mhe. Kaluma, kwa kusema haya, na naunga mkono kama vile Mhe. ambaye ameongea sasa hivi, lakini twahitaji tuupige msasa Mswada huu. Nikisema twahitaji tuupige msasa Mswada huu, ni kama vile wewe ulivyozungumza, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ulizungumza ukasema Kaunti ya Homa Bay, tukiiangalia, ilipewa shilingi milioni sita peke yake, na mimi, Jomvu, Mhe. Rozaah Buyu alipokuwa kamishina kwa ile tume ya Andrew Ligale, alikuja kule na tume yake yote, wakaja wakaona Jomvu yatakikana kukatwa kutoka kwa Changamwe. Mwaka 2013, Jomvu ikaweza kukatwa kwa sababu kulikuwa hakuna maendeleo; yakiangaliwa, maendeleo ilikuwa uongozi wakati ule ulikwenda katika sehemu ya Changamwe peke yake. Namshukuru Mhe. Rozaah Buyu baada ya 2013 kunikatia constituency ile pamoja na Andrew Ligale. Mwaka wa 2017 alikuja Bungeni na akaweza kuhudumu kwa vipindi viwili mpaka sasa tunafanya kazi na yeye. Kwa hivyo, hii Equalisation Fund yenyewe, kama vile inavyozungumziwa kwa Kiswahili, tunaweza kusema ni Mswada ambao unataka kuleta usawa. Na katika kuleta usawa, ni kwamba maana ya usawa ni kumaanisha eneo bunge lako, Mhe. Kaluma, liwe sawa na eneo bunge la Jomvu, na eneo bunge la Mhe. Farah Maalim, na eneo bunge lingine. Hapa tunaona imesemekana ni kaunti 14 peke yake, lakini nataka kuzungumza kitu leo tofauti kabisa. Katika kaunti 14 hapa hakuna kaunti yetu ya Mombasa, na ukiangalia kaunti ya Mombasa, wengi sana wanafikra ya kuwa ni kaunti ambayo ni ya kidosi, na watu wana pesa, na kila kitu kiko sawa, na iko mjini. Leo, ukiangalia katika eneo bunge langu la Jomvu, shida kubwa sana ambayo inakumba watu wangu wa Jomvu ni mambo ya ukosefu wa maji; mpaka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}