GET /api/v0.1/hansard/entries/1520329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520329,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520329/?format=api",
"text_counter": 320,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": ". Rais William Ruto aliamua kututengenezea ile barabara lakini wahusika wa kutengeneza barabara hiyo wanambwaga Mhe. Rais kwa kipande kidogo cha Jitoni ambacho hawataki kumaliza kwa sababu ya mambo yao wenyewe. Kamati ya Petitions ikiongozwa na Mwenyekiti wake ilikuja mpaka hapo. Walikuja mpaka pale, wakaangalia, na wakaona kweli barabara ile yatakikana kutengenezwa. Barabara hiyo yaunganisha Kilifi. Barabara ya Dongo Kundu yaanzia Jomvu yangu kwenda hadi kuunganisha Kwale. Constituency yangu yashikana na Kaloleni na Mvita. Kwa hivyo, tusiangalie Mombasa tu kuhusu fedha hizi za Equalisation Fund . Likoni kwa Mhe. Mishi ni mfano. Mwisho ni Kwale ukiingia Likoni. Hizi ni sehemu ambazo zinahitaji barabara na mambo mengi sana. Katika kawi, sehemu nyingi sana hazijafikiwa. Hakuna kawi katika Mbuyu wa Chapa ndani ya eneo bunge langu. Nenda Mireroni ambapo nimejenga mpaka shule ya JuniorSecondary School, hakuna kawi. Twatengeneza shule za Competency-Based Curriculum"
}