GET /api/v0.1/hansard/entries/1520331/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520331,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520331/?format=api",
    "text_counter": 322,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "ambapo twatakikana kuanzisha programu za kompyuta lakini hakuna kawi. Tutazifanya na nini bila kawi? Wenzetu wamenena. Wamesema zaidi juu ya haya. Kila kiongozi anavuta pesa hizi kwake. Unaona watu wengine na viongozi kutoka sehemu zao pia wanakuwa victims of circumstances . Tumeona kuwa wao pia wanafanyiwa dhuluma. Mhe. Kiborek ni mfano. Amesema kuhusu Baringo ambapo Moi alitoka. Kwa hivyo, Serikali zilizofuata zilifikiri kuwa Baringo haihitaji lolote kwa vile Moi alikuwa sehemu ya pale. Kaunti ya Mombasa pia yafaa iingizwe katika hizi kaunti kumi na nne na ipigwe msasa. Kaunti ya Mombasa haina ukulima na hakuna madini. Ni lazima you provide services au ufanye kazi ndani ya Kaunti ya Mombasa ilhali kazi hakuna. Vijana hawana kazi. Vijana wazunguka tu. Vijana wakienda kwa makampuni wanaambiwa hakuna kazi tangu Corona . Watu wasitupake mafuta katika maswala haya. Sisi pia tunaumia. Sisi pia tunastahili kupata mkate kama wengine wanavyopata mkate ndani ya Kaunti ya Mombasa. Nachukua fursa hii kutoa rambirambi zangu kama Mjumbe wa Jomvu. Kwa niaba yangu mimi, familia yangu, na wananchi wangu wa Jomvu, natoa rambirambi zangu kwa familia wa Seneta wa Baringo, Mhe. William Cheptumo, ambaye tulifanya naye kazi katika Bunge hili. Vilevile, natoa rambirambi zetu kwa familia ya Mhe. Malulu Injendi, Mbunge wa eneo Bunge la Malava. Mhe. Injendi alikuwa mtu wa busara sana. Busara yake ilionekana mpaka kwenye kifua chake na akitembea. Uliona msalaba alioweka kifuani. Hakuwa kama watu wengine wakitembea. Wengine hupanua vifua wakitembea. Yeye alimuweka Mungu mbele akitoa ushauri. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Lakini twaomba pesa hizi. Homa Bay County isipewe milioni sita kama ilivyopewa wakati ule. Uongezewe hata wewe, Mhe. Spika wa Muda. Nakutetea pia hapa. Vilevile, Mombasa tuwekwe ndani tupate pesa hizi. Kwa haya mengi, nakushukuru. Nashukuru kurekebishwa na kuongozwa na Mhe. Farah Maalim ambaye ni mzee wangu. Asante kwa kunipa nafasi hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}