GET /api/v0.1/hansard/entries/1521532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521532/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia kauli mbili ambazo zimeletwa na Sen. Olekina pamoja na Sen. Kibwana. Nitaanza na kauli ya Sen. Olekina. Matatizo yaliyotokea kutokana na uagizaji kutoka nje wa ngano imetokona na kutojua kwa watu wetu kwenye Wizara ya Ukulima na kwenye Wizara ya mambo ya nje. Yale makubaliano yanayofanyika katika vikao vinavyofanyika mara kwa mara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Yale yanayozungumzwa katika vikao vile hayafiki mashinani kwa wananchi. Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa inafaa iingilie kati kutatua suala hili. Wakulima wa nchi jirani wanajua masoko yao yako vipi. Wakulima wetu hawana habari hizo. Kwa mfano, mara nyingi sukari ya Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA) inaletwa nchini ilhali tuna sukari yetu nchini. Pia mahindi inatolewa sehemu za Malawi kuingia Kenya lakini bidhaa hii inapandwa kwa wingi na hatuwezi kununua kwa bei ambayo Serikali inaamua. Hivi sasa kumechaguliwa wenyeviti wapya wa kamati, inafaa waangalie kwa makini masuala haya ili wananchi wajue taarifa kuhusu mazao. Chakula tunacholima lazima kwanza kinunuliwe hapa kwetu, kile ambacho ni kizuri labda tuuze nje. Tusiwe tunaleta kila zao kutoka nchi, kwani tutawahujumu wakulima wetu. Afya ya akili ni suala ambalo liko wazi katika jamii zetu. Mara nyingi utapata mtu amejiua ama ameadhiri familia yake. Juzi kuna mama mmoja aliua watoto wake watatu hapa Nairobi. Kuna visa vingi kama hizi ambazo zinaripotiwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}