GET /api/v0.1/hansard/entries/1521535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521535,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521535/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Ni jambo la fedheha wakati wakulima wanapanda, kupalilia mimea na wanapovuna hawapati walichokuwa wanatarajia. Hili ni jambo linalotokana na makadirio ya bajeti ambayo yanafanywa na Bunge la Kitaifa. Sasa hivi ukiangalia fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kununua mahindi utapata kiasi. Ukiangalia fedha kwenye bajeti ambazo zimetengwa kwa sababu ya ngano, utapata hakuna. Pia hakuna pesa zilizotengwa kusaidia wakulima wa mimea mingine. Wakati wakulima watavuna, hata Mhe. Rais wa nchi atasema nendeni mnunue ngano. Hata hivyo, kwa sababu wakulima hawa hawana soko, utapata kuwa hakuna bajeti. Jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna mahali Seneti inahusishwa kikamilifu katika makadirio ya bajeti. Tunafaa kuweka fikira zetu pale ili tuwasidie watu wetu. Bw. Spika, siyo ngano na mahindi pekee. Vile vile kuna sheria zingine katika nchi hii ambazo zinahitaji Waziri kuhakikisha kuwa wakulima wamefaidika. Nchi zingine zinaruzuku wakulima wao kuuza bidhaa zao kwa bei rahisi katika nchi ya Kenya. Sisi tumekuwa kama jaa la kununua kila kitu kwa sababu bei ni rahisi. Ningependa kuzungumzia mazao ya makadamia. Ningependa kwanza kumpongeza Sen. Wakoli ambaye sasa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Tulienda naye kwenye ofisi ya aliyekuwa Waziri, Mhe. Mithika Linturi, kwa sababu kuna sheria ambayo ilikuwa imebuniwa mwaka 2023 ambayo ilikuwa inasema lazima utoe maganda kwenye makadamia kabla ya kuuza katika nchi za nje. Mabwenyenye waliungana na kujenga viwanda vikubwa vikubwa. Maskini lazima angepeleka mazao yake kule. Sasa hivi, kuna sheria hiyo kwamba mkulima hawezi kuuza makadamia nje ya nchi kama haijatolewa maganda. Kwa nini mkulima asiruhusiwe kufuga mbuzi wake mahali kuna nyasi? Kwa nini nilime kisha nikuletee kwa lazima kuambatana na sheria? Hilo ni jambo la kufedhehesha. Ni vizuri wakulima wa ngano waangaliwe haraka iwezekanavyo. Inafaa kuwa hivyo hivyo kwa wakulima wa mahindi na wengineo."
}