GET /api/v0.1/hansard/entries/1521564/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521564,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521564/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, kabisa nataka kuchukua fursa hii kutuma risala zangu za rambirambi kwa familia, jamii na marafiki wa Leonard Mambo Mbotela. Bw. Spika, itakumbukwa kwamba mtangazaji Leonard Mambo Mbotela alikuwa ni ngwiji wa Kiswahili. Nilimuenzi na hata kukipenda Kiswahili kwa sababu yake na watangazaji wengine kama Billy Omala, Njuguna Gatei pamoja na Mohammed Juma na wale wengine. Kusudi la kumpenda ni kwa sababu yeye alifanya kazi nzuri ya kuikosoa jamii na kile kipindi chake cha “ Je, huu ni ungwana ?” Jambo ambalo lilionekana kwamba halikukubalika katika jamii, alikuwa ni mwepesi wa kukosoa bila kuogopa. Bw. Spika, ninakumbuka kwa wakati ule aliweza kuwakosoa wazee wakati ambapo walikuwa wamepewa bonus . Ilitokea kwamba mzee alikwenda akajivinjari na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}