GET /api/v0.1/hansard/entries/1521565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521565/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "mvinyo hata hakuenda nyumbani na kutosomesha watoto. Alikuwa akiuliza “je, huu ni ungwana kwa nyinyi wazee, baada ya watoto na mama kufanya kazi ngumu lakini baada ya kupokea malipo, unapata hakuna manufaa yoyote.” Hayo maswali pengine angelikuwa hivi leo angeuliza, “Je huu ni ungwana kwa wakulima wa Narok kufanya kazi ngumu ya kukuza ngano na hatimaye kutoweza kuiuza? Hayo ni maswali ambayo aliyafanya kwa kuweza kuikosoa jamii. Sio hivyo tu, aliweza kutangaza mpira. Vilel alivyokuwa akitangaza mpira na alivyokuwa akitohoa maneno, niliweza kujua mambo mengi pale. Hii ni kwa sababu alisema hasa sisi, Wakikuyu, tuna ile shida ya lahaja. Aliweza kufafanua vile ambavyo ungeweza kutoathiriwa na lugha ya mama. Hiyo ndiyo lahaja. Ninamuona Seneta wa Mombasa ameniangalia. Kwa hivyo, aliweza kuelezea vile ambavyo ungeweza kuongea lugha ya Kiswahili. Pengine nikamwiga na nikaweza kupata mambo mawili au matatu. Nikimalizia nakumbuka vile ambavyo alikuwa akisoma taarifa zake na vile alivyokuwa akiongea. Nakumbuka akisema vile ambavyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Kenya alipokuwa mwaka wa 1982 wakati yeye mwenyewe alipokuwa Kenya Broadcasting Corporation (KBC) ama Voice of Kenya (VOK) na vile alivyoshambuliwa. Aliweza kusimulia na ukisikia akisimulia ile hadithi, unaipenda. Kwa hivyo, siku ya leo sisi tunamsherehekea na tunamuenzi. Pengine vile Seneta wa Nandi alivyosema ---"
}