GET /api/v0.1/hansard/entries/1521570/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521570,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521570/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Thang’wa",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hio ni sawa. Sasa inayoweza kufanyika kwa haraka ni sisi sote kujadilia hii Hoja kwa lugha ya Kiswahili, ambayo Mambo Mbotela alikuwa anatumia kutangaza. Tulipokuwa tunakua, huyu muungwana alikuwa kielelezo cha kuigwa. Baada ya masomo yangu, niliiingia katika chuo kusomea utangazaji. Nimekuwa mtangazaji kwa miaka zaidi ya saba. Alikuwa kielelezo cha kuigwa na wengi wetu tulipenda vile alikuwa akitangaza. Kama vile Seneta wa Kaunti ya Laikipia amesema, wengi wetu sisi ambao tumetoka “murima”, tuna shida ya matamshi ya ‘l’na ‘r’, ambayo wiki iliyopita iliniweka kwa shida wakati niliposema looting, kumbe nilikuwa namaanisha routing . Tulipokuwa tunamsikiza, tulikuwa tunamuiga alivyokuwa akisoma taarifa ya habari, akiuliza “ Je, huu ni ungwana ?” na tunazunguka kwa kijiji tukisema vilevile. Kwa hivyo, alitusaidia sisi ambao tulikuwa tunamsikiliza kurekebisha ama kufanya Kiswahili chetu kiwe sanifu. Nasema pole kwa familia. Ningalijua hii Hoja ilikuwa yaja leo, tungeweka watu wengine wengi kule ndani ambao pia walitoa huduma kwa taifa hili kama Wafula Chebukati. Tungemweka pale kwa sababu pia yeye ametoa huduma kwa taifa hili. Tungeongezea wengine ili tulete masikitiko na rambirambi zetu. Bw. Spika, naunga Hoja hii mkono."
}