GET /api/v0.1/hansard/entries/1521572/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521572,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521572/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Mhe. Spika, kwanza ningependa kumkosoa Kiongozi wa Walio Wengi kwamba haijachukua siku zaidi ya kumi tangu tumzike Mhe. Leonard Mambo Mbotela. Tulimlaza pale Langata tarehe 15 mwezi huu. Najua Kiongozi wa Walio Wengi labda hiyo tarehe inakuchanganya kwa sababu ulikuwa katika maeneo ya Addis Ababa kwa shughuli ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa African Union Commission (AUC). Mnavyojua, mimi ni mtu wa mkono wa Mhe. Raila Odinga. Kwa hivyo, nilisalia hapa na tukajiunga pamoja na mwakilishi wa kina mama wa Kaunti ya Jiji Kuu la Nairobi, Mhe. Esther Passaris, pamoja na familia ya Mwenda zake Leonard Mambo Mbotela katika maombi pale All Saints Cathedral. Ilikuwa ni siku ambayo sote tulimkumbuka huyu shujaa wa utangazaji wa habari katika taifa letu la Kenya. Bw. Spika, kinachonishangaza ni kwamba unakuta Seneta kama Sen. Cherarkey anatumia fursa hii ambayo tunamuenzi mtangazaji mkuu katika taifa letu kuwakosoa waandishi wa habari. Mhe. Spika, habari unazochagua kuona ni u pto you, y aani, ni wewe utachagua ile channel utataka kwa sababu tulipokuwa tunakua, kulikuwa na kituo kimoja cha matangazo ambacho kilikuwa cha mama na baba. Wakati huu kuna vituo vingi. Ikiwa unaona kuna kimoja ambacho habari zake zinakukera, uko huru wa kubadilisha mitabendi, kama walivyokuwa wakisema. Bw. Spika, ninavyojua ni kwamba, stesheni za kutangaza zitatangaza matukio jinsi ambavyo yalifanyika. Kwa mfano, leo Sifuna alirushwa nje ya Bunge la Seneti. Hautarajii kwamba waseme hakurushwa nje. Kwa hivyo, tuvipe vyombo vyetu vya matangazo nguvu ya kufanya kazi zao. Bw. Spika, tulikuwa na pendekezo mwaka wa 2007 kwamba tuwe na Heroes Corner katika kiwanja chetu cha Uhuru Gardens. Nimesema hapa mara nyingi kwamba kiwanja hicho kilitwaliwa na jeshi na mpaka sasa hatujaweza kufanya kazi hiyo ya kuweka Heroes Corner pale. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}