GET /api/v0.1/hansard/entries/1521579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521579,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521579/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
"speaker_title": "The Senate Majority Leader",
"speaker": {
"id": 13165,
"legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
"slug": "aaron-cheruiyot"
},
"content": " Bw. Spika, najumuika na Maseneta wenzangu kutoa rambirambi na pia kumshabikia huyu mwanahabari ambaye ni tajika katika taifa letu la Kenya kwa kazi yake aliyoifanya kwa ustadi hadi alipofikia. Kila mwanafunzi wa masomo ya uanahabari, waliokuwa wakati ambapo alikuwa kazini na hata alipostaafu, walikuwa wanatamani wafanye kazi alipofanya. Kwa hivyo, najumuika na wenzangu kutoa pole zetu kama Seneti. Pili, najumuika na Wakenya wote ambao walimshabikia na kusema asante, heko shujaa wetu kwa kazi ambayo umeifanya kwa hali ambayo imewafurahisha Wakenya wote na kusema kweli hapa kulikuwa na mwanahabari. Siyo kila siku ambapo tunapata mtu ambaye baada ya kutuaga, watu wanamshabikia na kusema “Huyo, katika kazi zake, alifanya ilivyotakikana.” Pengine kuna wengine wanajiuliza itakuaje baada ya siku karibu kumi vile tulivyoelezwa na kiongozi, Seneta wa Jiji Kuu la Nairobi, kwamba imekuwa ni siku kumi tangu walipomlaza ndiposa Bunge inazungumzia maswala haya. Ni kwa sababu kazi yake hata baada ya karne kumi bado itakua inakumbukwa katika taifa hili. Jambo la mwisho, nimesikia Maseneta wengi wakitoa mawazo kwamba ingekuwa vizuri kama tungekuwa na Heroes Corner ya kuwashabikia mashujaa wetu. Sisi kama Seneti tunafaa kuwa na kumbukumbu yetu, hata siyo Bunge kwa jumla. Wakenya ama binadamu yeyote ambaye amefanya mambo ambayo sisi kwa kimo chetu kama Seneti tunaona kwamba wamechangia kufika mahali ambapo tunafaa tuwakumbuke. Kwa lugha ya kimombo inaitwa “ hall of fame”. Katika institutions mbalimbali duniani unapata sehemu ambayo wameitenga na kusema kuwa kulingana na sisi tunaona bwana fulani amefanya mambo yake vizuri na inabidi sisi kama chuo au wizara tuwe na kona yetu ya kuwakumbuka watu kama hao. Imefika wakati ambapo ni lazima tuwakumbuke wale ambao wametoa mchango mkubwa kuhakikisha kuwa taifa letu limekuwa bora. Inabidi tuanze na wale waliojitolea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}