GET /api/v0.1/hansard/entries/1521587/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521587,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521587/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Se. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Jambo la kwanza ni kuwatakia kila la heri wajane walioachwa nyuma, watoto pamoja na vitukuu wake. Tunayo imani ya kwamba Mwenyezi Mungu atailaza roho ya marehemu mahali pema walipolala wema. Ninamfahamu Bw. Leonard Mambo Mbotela kwa miaka mingi. Alikuwa ni mtu muungwana na hata hilo jambo la kusema “Je, huu ni ungwana” ni kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa na tabia zake ambazo ni za heshima na za ungwana. Alikuwa sio mtu wa kutaka fujo. Saa zote alijaribu ku - encourage jamii ili iweze kutenda vyema katika maisha yao. Kijiji cha Frere Town kule Kisauni ambako wazee wake walitoka ni mahali pa heshima. Ijapokuwa siku hizi kumekuwa na watu wengi, lakini panajulikana mpaka hivi sasa ambapo Mzee Mambo alipozaliwa. Jambo ambalo tunaweza kulifanya ili kukumbuka shujaa Bw. Leonard Mambo Mbotela ni kwamba Serikali iweze kuangalia kama itakuwa ni barabara moja, vile tunavyoona mashujaa wengi hapa wamepewa majina katika ya barabara za Nairobi. Bw. Leonard Mambo Mbotela ameishi katika Jiji la Nairobi wakati wake mwingi. Ingekuwa jambo nzuri ikiwa hapa Nairobi, Mhe. Sakaja akiwa Gavana wa Kaunti Kuu la Nairobi, kushirikiana na wenzake waweze kutafuta barabara nzuri ambayo inajulikana wazi kwa wakati wowote kama vile Harry Thuku Road ama Jomo Kenyatta Avenue ili kuona ya kwamba hata baada ya miaka mingi itayokuja jina la Leonard Mambo Mbotela liwe linajulikana. Iwapo hatutafanya hivyo, basi itakuwa sio ungwana kwa sababu yeye mwenyewe hapo alipo atauuliza, “je, huu ni ungwana ikiwa mimi niliwatendea haya yote nikawa ninawaeleza njia ya kuenda ni ipi na leo hivi hata hamuwezi kunikumbuka katika miaka yangu niliyokuwa na nyinyi nikijaribu kutengeza mazuri.” Tukikosa kujibu hayo maswali ninaona suluhu kubwa ni kuona ya kwamba tumemkabidhi barabara fulani iitwe jina lake ili liweze kuishi kwa muda mrefu katika fikra za Wakenya."
}