GET /api/v0.1/hansard/entries/1521596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521596/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Olekina",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 407,
        "legal_name": "Ledama Olekina",
        "slug": "ledama-olekina"
    },
    "content": "Leo hii tunaeka kumbukumbu ya milele tukimkumbuka marehemu Leonard Mambo Mbotela, mtangazaji ambaye tutamkummbuka kama mmoja wa aliyetumia ucheshi ili kukosoa maadili yetu kama Wakenya. Nakumbukuka vizuri nilisoma ya kwamba mwaka wa 1982 wakati wa mapinduzi hapa Kenya, aliwekewa bunduki na kulazimishwa kusema ya kwamba “serikali imepinduliwa.” Lakini alipomaliza, aliuliza, “Je huu ni ungwana?” Kumaanisha ya kwamba tunaweza kutumia ucheshi ili kukosoa wakenya kwa mambo wanayofanya. Ni lazima tuhakikishe ya kwamba kumbukumbu hizi za milele tunazozieka hazitabaki katika makaburi ya Langata. Ningeomba tuwaenzi na kuwaheshimu watu waliojitolea kutuweka vizuri kama wananchi wa Kenya. Lazima mwili wake ufukuliwe na kuzikwa mahali ambapo Wakenya wote watamkumbuka kwa miaka nenda, miaka rudi. Bw. Spika, nilimuenzi sana marehemu mpaka nikaenda kusomea uandishi wa habari. Nilipokuwa Marekani, jambo la kwanza nililosomea ni uandishi wa habari. Hiyo ni kwa sababu nilimuenzi marehemu Leonard Mambo Mbotela ambaye tunaweka kumbukumbu zake sasa. Nawatakia familia yake, jamii yake yote na Wakenya wote heri na fanaka wanapozungumza na kuweka kumbukumbu hii ya milele. Asante."
}