GET /api/v0.1/hansard/entries/1521599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521599,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521599/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Nyamu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nilifurahia kipindi hicho na nilikuwa nasubiria kwa hamu kipindi kinachofuata ili kujua angezungumzia nini. Marehemu alikuwa analenga sana tabia za jamii. Nakumbuka nilikuwa nikiangalia watu wazima kama wanafanya vitu vya ungwana kulingana na matarajio ya marehemu kama ungwana. Alichangia pakubwa kuunda tabia njema katika jamii. Wanahabari wengi wanakosa maadili hayo kwa uanahabari wao. Tungependa wanahabari waangalie jinsi wanavyosaidia jamii. Wasikubali kutumiwa na wanasiasa na watu wengine kwa sababu ya fedha. Asante, Mhe. Spika."
}