GET /api/v0.1/hansard/entries/1521601/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521601,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521601/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 277,
        "legal_name": "Kibwana Kivutha",
        "slug": "kibwana-kivutha"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Pia mimi naomboleza kwa kutoa rambirambi zangu na kuunga mkono ndugu zangu walioongea kuhusu kifo cha mtaalamu wa Kiswahili, mwandishi na mwanahabari, marehemu Mambo Mbotela. Bw. Spika, siwezi kusahau kuwa juzijuzi ni kama alikuja kutuaga. Alikuja tukazungumza na kupiga picha pamoja. Nakumbuka nikimtania na kumwuliza kana hapa kuna ungwana. Aliniambia, hapa kwa Bw. Spika kuna ungwana maana amenikaribisha. Kila nikikumbuka, chozi linanitoka kwa kumkumbuka. Wewe pia utakumbuka kuwa alipata nafasi ya kuja kuzungumza na wewe na kukuaga. Marehemu Leonard alitutumbuiza sote tukiwa nyumbani. Tulikusanyika sote kusubiri kipindi chake cha redio na televisheni. Alitufundisha Kiswahili. Marehemu Mbotela ameacha urithi mkubwa wa tasnia ya uandishi na uanahabari. Nakumbuka Sen. (Dr.) Oburu alivyosema kuwa alilazimika kutangaza kupitia televisheni kuwa Serikali imepinduliwa mwaka wa 1982. Alikuwa na roho nzito kufanya hivyo. Ilikuwa jambo gumu kwake kushikwa kwa nguvu kutangaza hayo. Mchango wake utakumbukwa sana vizazi na vizazi vijavyo, kipindi chake pamoja na jinsi alivyotuonyesha umahiri wake kwa uanahabari. Tunaomba Serikali iwapatie familia yake nafasi yoyote serikalini na iwasaidie kwani kuna mjane aliyeachwa. Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi penye wema. Asante."
}