GET /api/v0.1/hansard/entries/1521602/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521602,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521602/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii kuhusu mzee wetu Leonard Mambo Mbotela ambaye alikuwa maarufu. Alijulika nchini na pia nchi za Afrika mashariki. Tulipokuwa wachanga, Kenya Broadcasting Coorporation (KBC) ilikuwa inafungulia saa kumi na moja na kufunga saa tatu usiku. Kabla habari za saa moja, kuna wakati Leonard Mambo Mbotela angesoma habari. Ni mzee mmoja aliyejulikana kwa sifa zake nzuri. Alizaliwa sehemu za Frere Town. Naomba Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, Gavana wa Mombasa na Wabunge kutoka Kaunti ya Mombasa, haswa Kisauni, shule inayoitwa Frere Town wabadilishe jina iitwe Leonard Mambo Mbotela Primary School Free Town kwa sababu kwao ni Free Town. Bw. Spika, sio vibaya kubadilisha jina la shule. Jina hili litahusishwa na shule hii milele. Vitukuu watajua kulikuwa na shujaa aliyekuwa akitangaza katika redio. Leonard Mambo Mbotela alikuwa anajulikana sana. Wakati wake kulikuwa na watangazaji wengine kama Ali Salim Manga, yuko hai. Huyu alikuwa mtangazaji The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}