GET /api/v0.1/hansard/entries/1521605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521605,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521605/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Oketch Gicheru",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, nachukua fursa hii kukupa pole, kwa kumpoteza babako. Naomba Mungu aipoze roho yako. Pili, kama kijana nchini, mimi hutazama mbele wakati ambapo sisi kama Wakenya tutakuwa na maadili mema. Katika Katiba yetu, Sura ya Sita, kuna maadili ambayo imeashiriwa. Natazamia siku moja ambayo Wakenya watakuwa na maadili mema. Namkumbuka marehemu Leonard Mambo Mbotela kwa kipindi ambacho alikuwa anatangaza. Kipindi hiki kiliangazia maadili ya jamii. Licha ya kuwa na Serikali na polisi, inawezekana jamii iwe na maadili mema. Kipindi cha “Je, huu ni ungana.” hakikuwa kipindi tu kwangu. Nimekitazama kwenye Youtube . Kipindi hiki kiliangazia maadili mema katika jamii. Hapa nchini watu hawana maadili. Wanasiasa wako na changamoto ya tamaa. Inafaa wanasiasa wasome kutokana na mafunzo ya Leonard Mambo Mbotela. Wanafanyi biashara pia hawama maadili. Waendeshaji pikipiki na matatu hawana taadhima wala utu barabarani. Masuala haya ndio Leonard Mambo Mbotela alikuwa anayezungumzia. Tunapoomboleza ndugu yetu, naiombea familia yake mema. Naomba Mungu awafariji. Kama taifa, tuzingatie yale aliyokuwa akiyasema kwenye kipindi chake. Na tusikuwe na tamaa---"
}