GET /api/v0.1/hansard/entries/1521609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521609,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521609/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Korir",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Nachukua nafasi hii kutoa risala za rambirambi kwa Spika kwa kupoteza baba mzazi. Poleni sana. Tumepoteza viongozi ambao wamefanya kazi ya kuifunza jamii na kuitunza familia. Siku ya leo tunashuhudia matunda ya kazi yao. Leonard Mambo Mbotela alikuwa na kipindi ambacho alitumia kufunza Wakenya mambo mengi. Kuna mambo mengi ambayo yanaendelea hivi sasa yanayoshtua jamii. Tabia ambazo ziko kwenye mitandao haziandamani na maadili ya kijamii. Leonard Mambo Mbotela alifanya kazi nzuri. Alichangia kwenye michezo. Tumempoteza mtu mashuhuri. Pole kwa familia na nchi nzima. Asante, Bw. Spika."
}