GET /api/v0.1/hansard/entries/1521616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521616,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521616/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kushukuru na kuwapongeza Maseneta wote ambao wamechangia Hoja hii. Shukrani maalum ziwaendee Maseneta wafuatao: Sen. Cherarkey, Sen. Kinyua, Sen. Ogola, Sen. Thang’wa, Sen. Sifuna, Sen. Cheruiyot, Sen. Madzayo. Sen. Veronica Maina, Sen. Olekina, Sen. Nyamu, Sen. Kibwana, Sen. Oketch Gicheru, Sen. Korir na Sen. (Dr.) Oburu kwa michango yao. Ni wazi kwamba mchango wa mwendazake Leonard Mambo Mbotela ulikuwa mkubwa sana kwa taifa letu. Hivyo basi, haitakuwa sawa kutofanya jambo lolote litakaloweka jina lake katika nyoyo zetu milele. Kwa mfano, Sen. Boy wa Kwale amependekeza kuwa Shule ya Frere Town iliyoko katika Kaunti ya Mombasa ipewe jina la Mbotela. Vile vile, pale Frere Town kuna ukumbi ambao unaweza kupewa jina lake. Hiyo inaweza kufanyika pia Nairobi kwa sababu hapa ndipo alifanya kazi kwa muda mrefu. Bw. Spika, ipo haja ya kuwa na kigezo kitakachotumika kukumbuka jina lake. Tunaiombea roho yake iwekwe mahali pema peponi."
}