GET /api/v0.1/hansard/entries/1521657/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521657,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521657/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Jambo la kwanza yule ambaye alikuwa amefanya makosa na ikabainika wazi ya kwamba kweli Seneta alikuwa amefanya makosa, aliweza kuomba msamaha wakati alipatikana kuwa na hiyo hatia. Kwa kawaida unaona ule ugumu wa mtu akiwa amekosea na akiwa hajui, na akiwa amekosea na akiwa anajua. Wengi huwa pengine wanaweza kukataa kuomba msamaha ama wengine wakaweza kuomba msamaha. Sasa hivi tayari ndugu yetu Omtatah alikuwa hapa na amesema ijapokuwa akijivua yeye nguo yake anaweza kuomba msamaha, lakini kwa vile ambavyo ameona ajigawanye mara mbili, akasema yeye pia amesema pole sana na anaomba msamaha na hii Seneti ikamsamehe."
}