GET /api/v0.1/hansard/entries/1521662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1521662,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521662/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kila binadamu hufanya makossa. Vile vile huwa anaweza kuomba msamaha ama kukataa kuomba msamaha. Dada yetu Orwoba Gloria aliomba msamaha. Kwa hivyo, sioni jambo gumu ya kwamba kutakuwa na mushkil ambao hatuwezi kumsamehe. Nimeona siku alizopewa, 79, za kuadhibiwa. Alipooamba msamaha, sisi wote tulikuwa na mioyo mikunjufu na tukakubaliana. Naona ya kwamba kuzipunguza siku hisi ili dada na Seneta mwenzetu arudi, hakuna shida. Naunga mkono hii Hoja ya kugeuza kutoka siku 79 hadi 30, ili dada yetu arudi katika Bunge hili la Senate aendelee kama kawaida yake, kusaidia Wakenya katika maisha yao. Asante, Bw. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii."
}