GET /api/v0.1/hansard/entries/1521675/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1521675,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521675/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Hii ni kwa sababu unapofanya makosa na kuyajutia, unapaswa kumuomba msamaha yule ambaye ulimkosea ili naye aweze kukubali msamaha huo. Sisi kama Seneti tunaweza kukubaliana lakini yule ambaye aliadhirika bado yuko na uchungu. Ni vizuru Sen. Orwoba amuombe msamaha yule ambaye aliathirika kwa sababu Kitabu Kitakatifu cha Mungu kinasema kuwa kile ambacho kimesamehewa humu duniani, hata mbinguni kimesamehewa. Mimi ninakubaliana na wenzangu lakini kwa sababu yule hakosei ni mia kwa mia ni Mungu peke yake. Ni vizuri hata sisi tusamehe kwa sababu leo ni mimi, kesho ni wewe. Ni mtindo mzuri kwa watu kusameheana tukiwa katika dunia hii, ninaweza nikakukwaruza na kesho unikwaruzwe na mwingine. Ule uzoevu wa kusameheana utakuwa ni mfano mzuri katika nchi yetu ya Kenya. Tumekuwa tukijadili hii Hoja ya Bw. Leonard Mambo Mbotela, itakuwa ni ungwana kwetu sisi kuwasamehe wenzetu."
}