GET /api/v0.1/hansard/entries/1522053/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1522053,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1522053/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Ningependa kuchangia Taarifa kuhusiana na mambo ya mahakama ambayo imeletwa na Sen. (Prof.) Ojienda. Kumeingia mtafaruko katika Tume ya Mahakama kutokana na kesi ambazo zimepelekwa mahakamani na Majaji wa Mahakama ya Upeo (Supreme Court) ambayo inahusiana na masuala ya hatua za nidhamu ambazo zilikuwa zichukuliwe na Tume Uajiri wa Majaji. Ni masikitiko kuwa Jaji Mkuu pia ameenda mahakamani kuzuia Tume ambayo anaiongoza kuchukua hatua za kinidhamu kuhusiana na madai ambayo yameletwa kwa Tume hiyo na baadhi ya mawakili wakuu katika nchi hii yetu ya Kenya. Sio jambo la sawa kwamba kiongozi wa Tume anapeleka kesi mbele ya majaji ambao wanaajiriwa na Tume hiyo. Ijapokuwa majaji wanao kinga ya kikazi, inakuwa sio sawa kwa sababu majaji wale wanamuangalia Jaji Mkuu kama mtu ambaye ni kiongozi wao. Na labda hawawezi kutoa amri ambayo ni kinyume na maombi ya Jaji Mkuu. Masuala haya ni mazito na ninafikiria itataka kamati husika ya Sheria na Haki za Binadamu kulivalia njuga suala hili kwa haraka kwa sababu, ni jambo ambalo litaweza kupunguza imani ya wananchi katika mahakama zetu. Ikiwa mtu ana tuhuma ya kwamba jaji fulani ameamua ama amepokea hongo ama amefanya mambo kinyume na maadili ya kikazi, ni muhimu masuala hayo yachunguzwe kwa haraka ili uamuzi uweze kupatikana. Itakuwa sio sawa jaji yule aendelee kuhudumu wakati tume inavuruta miguu kusikiliza madai yale na kuamuru kwamba hakuna mashtaka ama pengine mashtaka yapo na watoe mapendekezo kwa Rais aweze kuweka tume ambayo itaweza kuchunguza jaji yule kwa haraka iwezekanavyo. Haya masuala ambayo yako sasa, yanapunguza imani ya wananchi katika mahakama zetu. Kwa hivyo yanafaa yachunguzwe kwa haraka na Kamati yetu ya Sheria na Haki za Binadamu ili iweze kujulikana usawa uko pahali gani. Asante sana Bw. Spika."
}