GET /api/v0.1/hansard/entries/1522445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1522445,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1522445/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Masara. Mswada huu unalenga kuboresha ustawi na hadhi ya askari wetu. Polisi wetu wanaishi maisha ambayo unaeza dhani wao si binadamu au watu ambao wanatangamana na binadamu. Askari wetu hapa Kenya wana dhiki, hii ndio lugha ambayo naweza tumia ili niweze kueleweka vizuri. Wana dhiki, shida na maisha magumu wakati ambapo wanatuhudumia na pia baada ya kustaafu. Mswada huu unalenga kudumisha ustawi wao na hadhi yao. Utaweza pia kuwatengea kitengo maalumu cha kuweza kuwashughulikia askari hawa ambao mara nyingi wanapatikana na shida ya msongamano wa mawazo na madhara ya akili. Wanafanya kazi ngumu sana. Unaweza hata kupata askari amefanya kazi hata masaa 24, akikimbia juu na chini. Mara nyingine unapata ameitwa mahali ajali imetokea ambapo hata wewe binadamu wa kawaida huwezi kuangalia yale mazingira ambayo ajali ile imetokea kwa sababu pengine labda mtu ameumia sana ama amekufa kifo kibaya sana. Na sijaona askari akisonga mbali na hali kama hiyo. Wengine unapata wanaenda kuokoa mahali kuna mkasa wa moto na anapambana na mambo mengi. Mazingira ambayo askari wetu wa Kenya wanaishi ni ya aibu. Ni ya aibu hata ukiyasema kwa mataifa mengine na pia kwa Wakenya. Wanaishi maisha ya kinyama. Unapata askari amepatwa na msongomano wa mawazo kwa sababu hata anashindwa kutunza familia yake kwa sababu mshahara ni duni, hawezi kupata matibabu mazuri na pia hawezi kupatia watoto wake elimu nzuri. Maisha ikiwa hivi, askari watajihusisha na mambo mengi. Wengi wanaingilia ulevi na kuwa mlevi mkubwa kwa sababu anawaza ameshinda kazi kuanzia asubuhi mpaka jioni lakini mwisho wa mwezi mshahara wake hauwezi kumtosha hata wiki moja. Anakopa na kujipata mwisho wa mwezi analipa madeni tu na anaanza tena kwa kijiti; yaani anaanza moja tena. Anakopa mpaka ifike tarehe thelathini, akipata mshahara, analipa madeni yale na kuendelea kuishi. Je, haya ni maisha ya aina gani ukilinganisha na kazi ambayo askari wetu wanayoifanya ndani ya taifa letu? Naunga mkono Mswada huu ili iweze kudhibiti. Askari ni baba zetu, dada zetu, na marafiki wetu na tunaishi nao vizuri. Pia wanatufanyia kazi nzuri zaidi. Ninaunga mkono Mswada huu. Natumaini itapitishwa na Bunge hili iweze kusaidia ndugu zetu. Mhe. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa fursa hii."
}