GET /api/v0.1/hansard/entries/1523397/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1523397,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1523397/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Ni lazima wawekewe bima. Wakati mwingine, wao hupata ulemavu wakienda kazini na kurudi manyumbani mwao kuteseka na familia zao. Watoto wao hawasomi vizuri kwa kuwa wanahamishwa hapa na pale. Inafaa wawe wanajengewa chuo cha maafisa wa polisi na watoto wao waishi pale kwa uzuri, ili maafisa wafanye kazi kwa utulivu. Hivi sasa, wanaishi katika hali ngumu sana. Wanalala katika sehemu iliyogawanywa na nguo ya aina ya leso tu! Mmoja yuko upande huu na mwingine upande ule. Wakati mwingine, mmoja anapewa zamu ya usiku ilhali afisa mwenzake anabaki pale nyumbani. Saa nyingine, wake wa wengine wamehama na wako nao pale. Utaenda kufanya kazi namna gani? Si hapo ndipo panatokea sababu ya kupiga risasi ovyo? Kwa hivyo, ni kweli ni lazima maslaha ya hawa watu yaangaliwe. Nao pia wafanye uaminifu ili wananchi wakubali maafisa hawa wanashika watu kwa makosa ya kweli. Namshukuru ndugu aliyeleta swala hili la kuangalia maslaha ya polisi."
}