GET /api/v0.1/hansard/entries/1523628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1523628,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1523628/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kutoa maoni kuhusu kauli ya Sen. Catherine Mumma kuhusu janga la madawa ya kulevya, hasa kwa vijana wetu. Wakati husika inaangalia suala hili, wajaribu pia kuangalia vile hali ilivyo, hasa wakati wa likizo. Hii ni kwa sababu wananchi wengi wanajua ya kwamba – na hasa katika kaunti yangu – watoto wanajifunza kula miraa, kuvuta sigara wakati wa likizo. Tunataka kujua wakati huu Kamati inafanya investigation yake, wajaribu pia kuangalia ni pesa ngapi zinazotumika na NACADA kwa upande wa mashule. Ni vipi ambavyo bajeti hii inaweza kutumika kwa upande wa mashule ili watoto waweze kufunzwa heshima na namna ya kuishi bila matumizi wa madawa ya kulevya. Kuna wakati ambao, aliyekuwa makamu wa Rais, alikuwa anahusika sana na suala hili. Tungependa kujua hicho kitengo ama zile pesa ambazo alikuwa anafanya mikutano nayo, zilikuwa ni pesa ngapi, zilitumika sehemu gani – kwa sababu inaonekana kama baada ya yeye kuondoka, hiyo programme imenyamaza. Tunataka kujua nani anashughulikia suala hili la watoto wetu wakipotea kwa mambo ya madawa ya kulevya, hasa wakati shule zimefunga na watoto wako kwa likizo."
}