GET /api/v0.1/hansard/entries/1523634/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1523634,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1523634/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ninaunga mkono taarifa ya Sen. (Dkt.) Murango kuhusu bima ya afya ya walimu. Ni jambo la kuvunja moyo sana ikiwa walimu wetu ambao wanafanya kazi kwa bidii sana, halafu unapata hatimaye akienda hospitalini, hawezi kupata matibabu kwa sababu bima yake haijalipwa. Sio hayo tu, taarifa iliyoletwa na Sen. Cherarkey inasema ya kwamba ukitembelea hospitali zetu hakuna dawa ilhali sisi kama Seneti tumegawa pesa na kuzipeleka katika kaunti zetu. Tunaonekana kama kwamba Seneti hatufanyi kazi yoyote kwa sababu nakumbuka juzi tu Seneta wa Narok, alileta Mswada hapa kuhusu madeni na tukapitisha lazima madeni hayo yalipwe. Ukienda hospitalini unaambiwa, dawa haziwezi zikapelekwa na KEMSA kwa sababu madeni hayajalipwa ilhali tunaendelea kupeleka pesa katika gatuzi zetu. Inaonekana ni kama zile pesa hazifanyi kazi ambayo zinapaswa kufanya. Kuna taarifa iliyoletwa na Sen. Mumma kuhusu mambo ya madawa ya kulevya na mihadarati. Seneta mmoja ameuliza kama aliyekuwa naibu wa Rais, Rigathi Gachagua, alienda na ile kikapu cha pesa aliyokuwa anatumia kupigana na mihadarati. Kwa hivyo---"
}