GET /api/v0.1/hansard/entries/1523635/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1523635,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1523635/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Mumma. Madawa ya kulevya ni janga ambalo limekumba nchi yetu kwa muda mrefu, hasa kaunti za pwani. Ukienda Mombasa, utapata madawa yameathiri vijana wengi. Hao huanza na madawa madogo kama muguka na zinginezo. Kwa hivyo, ipo haja ya kupambana na janga hili kikamilifu. Naibu Rais wa zamani alikuja Mombasa akalaunch vita dhidi ya madawa ilhali ilikuwa ni kama upepo wa kupita. Hii ni kwa sababu hatujaona jambo lolote kubwa ambalo limefanyika ili kupambana na madawa hayo baada ya uzinduzi huo. Serikali imeanzisha vituo vya kutibu wagonjwa kama ile ilioko kule Miritini. Pia, Serikali ya Kaunti ya Mombasa iko na kituo pale Frere Town lakini vituo hivyo havitoshi. Inapaswa swala hili liangaliwe zaidi kwa sababu hayo madawa bado yanauzwa katika hivyo vituo. Mambo ya usalama ni kazi ya Serikali kuu. Kwa hivyo, serikali za kaunti haziwezi kufanya lolote kupambana na mihadarati kikamilifu ikiwa polisi hawafanyi kazi yao. Kenya haina kiwanda cha madawa. Madawa haya yanaingia kupitia mipaka yetu ilhali kuna polisi na immigration and DCI officers . Kwa hivyo, bali na kamati---"
}