GET /api/v0.1/hansard/entries/1524024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1524024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1524024/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa ruhusa niweze kuchangia mambo ya mchele ya West Kano Irrigation Scheme katika Kaunti ya Kisumu. Ninashukuru watu wa West Kano na Patrick Ochieng ambaye hakujali maisha yake na mambo ya dunia. Chakula cha Mwafrika duniani na hata katika kaunti zetu 47 ni mahindi na wali. Tulienda kule Kano na hao wazee walitoka mbali lakini hawakujali. Hao watu walikuwa na shida nyingi. Waliposimama kutoa ushuhuda ilikuwa ni jambo la kuhuzunisha. Walikuwa wanaongea lugha ya Dhuluo. Hao watu hawakuwa na chakula lakini walijikakamua wakaja kutoa ushuhuda. Walisema jinsi pesa ambazo walipewa kutoka Japan zilikulwa na watapeli. Jambo la huzuni ni kwamba hao watu wa eneo ya West Kano huteseka sana mvua inaponyesha wanahama makazi yao kwa sababu maji kuloa kila mahali. Mvua inapokwisha, hao hurudi makazi yao kulima mchele. Watu walitoka nchi ya ng’ambo na wakawapea hela ambayo walitumia kulima mchele. Pia walipewa mashini ya kulima lakini watu watapeli walikula hiz pesa zote. Kenya imekuwa na shida nyingi sana. Mimi ni Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Agriculture, Livestock and Fisheries. Jana, tulisikia jinsi watu walipewa mahindi mbaya katika kaunti yako na wakakosa hata dawa ya ugonjwa ya mahindi. Hao wakulima hawakupata mavuno mazuri kwa sabaa mahindi yao yalivamiwa na wadudu. Kaunti nyingi zimekuwa na shida kwa sababu watu wakipewa kazi, wao hufikiria juu ya shida zao na familia zao. Hao hufikiria vile wataendesha magari na mashamba makubwa. Wao hujali tumbo zao kubwa. Ningependa sheria iangalie vizuri maofisa wa EACC ambao walikuwa wanafanya uchunguzu huu. Huenda EACC Act inahitaji ukarabati ili ipewe makali. Ingekuwa imara mambo kama haya hayangefanyika. Leo katika kamati yetu ya Labour and Social Welfare, tumeshuhudia professors ambao waliretire na hawakupata pesa yao ya uzeeni. Tumeona mambo mengi yakifanyika katika Serikali hii ya Kenya Kwanza. Tumeona mambo mengi na National Hospital Insurance Fund (NHIF) na Social Health Insurance (SHI). Juzi tumeona watu wengine wamekata kulipa deni. Walipoitishwa hela na Kenya Power (KP), hawakukumbuka ya kwamba kuna binadamu angeweza kupita barabara hiyo. Hawakufikiria kuhusu mazingira au kama kunaweza kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Walitupa takataka na kufunga barabara licha ya kupewa jukumu la kuzingatia usafi katika kaunti zetu. Mambo mengi yanaendelea kutendeka katika kaunti nyingi na sio katika kaunti ya Jiji la Nairobi pekee. Wanaoumia ni wananchi walio vijijini. Kuna janga la njaa na upungufu wa maji ya kunywa. Umeme au stima ni shida kwa wananchi wetu. Bw. Spika wa Muda, mwananchi anayelipa ushuru anafaa mahitaji yake ya afya, elimu, kilimo na barabara yatiliwe maanani. Serikali ya Kenya Kwanza inafaa kuangalia The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}