GET /api/v0.1/hansard/entries/1524025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1524025,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1524025/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ni wapi mambo haya yalishindikana ili tuyarekebishe. Mwananchi tajiri na maskini wote wako sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Bibilia inasema watu wawili hawawezi tembea pamoja bila kuelewana au kusemezana. Ningeomba tulio katika Serikali hii ya muungano inayoongozwa na Mhe. Rais Ruto na Naibu wa Rais, Mhe. (Prof.) Kindiki Kithure ambao wanahubiri umoja wa kitaifa tuwasaidie na tufanye kazi pamoja tukiwa na amani. Bw. Spika wa Muda, tumeona mambo mengi. Kuna wizi wa mashamba na magari. Watu wanapigana chenga. Tusipokuwa na heshima hatutatembea pamoja. Miezi miwili iliyopita, tulizuru Jamuhuri ya Tanzania. Wakenya wanafaa kuishi kama Watanzania kwa amani na umoja. Naomba Hoja hii izingatiwe kwa makini ili pesa zipatikane ili wazungu wale wafanye kazi inayohitajika waendelee kufanya hivyo. Tractors hizo ni za zamani sana na hazitumiki kwa sasa. Wale wazungu walisema hawatatupa pesa zingine kwa sababu ya ufisadi. Najua kuwa Serikali hii italipa mkopo huu wa pesa. Bw. Spika wa Muda, tumeona Serikali ikilipa deni ya sekta za sukari, kahawa na majani baada ya watu wengi kuililia. Kama tutaendelea kujenga barabara baada ya kupewa msaada kutoka nchi za ng’ambo na Serikali kuchukua ushuru kutoka kwa wananchi bila uwajibikaji, basi nchi itarudi nyuma miaka mingi. Kama uwajibikaji utazingatiwa, basi ajenda yetu kama nchi itasonga mbele. Watahakikisha kuwa katika sekta ya kilimo, wananchi watapata maji ya kufanya"
}