GET /api/v0.1/hansard/entries/1524027/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1524027,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1524027/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kutoka kwenye dams. Elimu itakuwa bora. Sekta za usafiri na afya pia zitaimarika. Mwezi uliopita nchi ya Amerika ilisema itakomesha utoaji misaada yote ya kiafya. Kama uwajibikaji ungezingatiwa basi tungekuwa na rasilmali za kutosha kuimarisha sekta ya afya yetu. Waheshimiwa wengi wako mashinani kwa sababu pesa zimekuliwa na matapeli. Ugonjwa wa saratani umeongezeka kwa kiwango cha juu. Watu wetu katika kaunti nyingi wamefilisika kwa sababu ya hali ya afya. Wameuza mashamba ili waweze kutibiwa. Hati miliki za mashamba yao zimechukuliwa na benki kwa sababu wana madeni mengi ya hospitali. Hatungekuwa tunapata shida hii ya ugonjwa huu wa saratani kama Serikali ingezingatia uwajibikaji. Kama Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo ya Mifugo na Uvuvi, tulitoa amri kuwa DCI wafanye uchunguzi ili watu hawa wapelekwe kortini na ukweli ujulikane. Haya sio mambo ya West Kano pekee yake yanahusu kaunti nyingi na inahitaji idara nyingi za Serikali kufanya kazi pamoja. Naunga mkono ripoti hii."
}