GET /api/v0.1/hansard/entries/1525419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1525419,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525419/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "shuleni kwa sababu ya wizi wa ng’ombe na migogoro ya mashamba. Kwa hayo, naunga mkono Taarifa ya Sen. Kinyua. Pia naunga mkono Taarifa ya Sen. Cherarkey wa Kaunti ya Nandi. Ni mara nyingi tumelalamika kuhusu kampuni ya Kenya Power and Lighting Company (KPLC). Sisi wanyonge na wale wengine tunalipia stima kila mwisho wa mwezi lakini kampuni kubwa hazilipii. Kaunti zote 47 zinahitaji usalama na zinahitaji kewekewa stima na KPLC lakini wamekuwa na shida kulipia. Naomba kufanywe upelelezi vizuri ili tujue kwa nini kile kitendo kilifanyika katika Kaunti ya Nairobi. Mji wa Nairobi ndio mzazi wetu. Walifanya kitendo kilichoonekana dunia nzima. Ni kama mtu ameenda kudai deni halafu unaenda kwa nyumba yake kumfungia nyumba na hakuna sheria kama hizo. Kilikuwa kitendo cha aibu sana. Tunajua kuna shida hapa na pale. Kaunti nyingi hazilipi madeni---"
}