GET /api/v0.1/hansard/entries/1525426/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1525426,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525426/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, kusema ukweli, tumekuja hapa kutetea wanyonge. Kwa hivyo, kama tumekuja hapa kutetea wanyonge, hata sisi ni wanyonge. Kaunti zote tunazopatia pesa ni matajiri na hawalipi KPLC pesa yao. Wakati kile kitendo kilipofanyika, kuna watu wa mazingira wako pale. Pia kuna magari hupitia pale. Kwa hivyo kungetokea vita, hakuna mahali watu wa usalama wangepitia. Tuko hapa kutetea wanyonge kwani ndio walionileta hapa ili niwatetee. Sikuwa nimekosea. Kaunti ya Nairobi ambayo Seneta wake ni Katibu Mkuu wa Muungano wa Azimio la Umoja aliyesimama kuongelea kisa hicho. Isipokuwa ametoka, angekuwa hapa aone vile Kaunti yake imefanya makosa. Kaunti nyengine zikifuata mkondo huo, itachafua mazingira na kudhoofisha usalama. Naunga mkono kwamba kutengenezwe kamati ichunguze kwa nini Kaunti ya Nairobi ilifanya kitendo kama hicho. Nimesikia akisema kwamba Seneti iko na pesa ya Kaunti. Huenda ikawa hajaitisha pesa halafu wanaenda kufunga barabara. Dawa ya deni ni kulipa. Ningeomba deni ya KPLC ilipwe na kaunti zote. Sio kaunti pekee ambazo hazilipi madeni ya KPLC, kuna wizara nyingi hazilipi madeni. Bw. Spika, naunga mkono kuwe na Kamati ya kufuatilia ili kuona vile watu watakuwa wanalipa pesa ya stima. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}