GET /api/v0.1/hansard/entries/1525589/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1525589,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525589/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hayati Rais Moi alikuwa anaongoza nchi. Tunakumbuka vizuri kulikuwa na Agricultural Extension Officers ambao walifunza watu kuhusu mmomonyoko wa udongo, kupanda miti na uchimbaji wa mitaro. Kilimo cha wakati huu kiko na shida. Tukishikilia kilimo vizuri, tutaishi vizuri kwani mtu akikosa mshahara na anaweza kuishi kwa pesa kidogo. Nakumbuka vizuri wakati tulichaguliwa mwaka 2022 kulikuwa na janga la njaa lakini Mungu akatusaidia na mvua ikanyesha. Nakumbua tulikuta unga wa mahindi ukiuzwa shilingi mia mbili na kumi. Wakati mvua ilinyesha na kilimo kikafanikiwa, unga sasa hivi unauzwa shilingi mia moja na thelathini. Kama Mungu alitusaidia, watu wa kilimo upande wa Serikali wangetusaidia kwa kutupatia mbegu nzuri, kuchimba mabawa ya maji na kutupatia pembejeo za kilimo cha mahindi, hatungesikia yale mambo yaliyofanyika katika kaunti hiyo. Tumechangia na kusema kwamba ni kaunti moja tu ya Bomet. Tunajua kwamba sio kaunti moja bali kaunti nyingi. Ni vile yule Seneta ameona hayo mambo yanaendelea huko kwao na yamefunikwa na hawakushughulika kujua watayatatua vipi. Naunga mkono ripoti ya Kamati ya Kilimo ambayo mimi ni Naibu Mwenyekiti. Tulichambua kisa hicho na tukasema kwamba wale watu wafidiwe. Bi Spika wa Muda, kuna bima ya kilimo. Hakuna mmiliki wa gari hupenda kulipa bima ili alipwe fidia. Vilevile, kwenye kilimo hakuna mkulima angependa kuweka bima ili apate fidia. Ningeomba Serikali inayotuongoza ya Kenya Kwanza iweke kipao mbele masuala ya kilimo, hasa upandaji wa mahindi. Mchele unapanwa katika Kaunti ya Kirinyaga na kaunti zingine pia. Hivi sasa kaunti ya Kirinyaga kuna wadudu wengi. Ilhali kuna agricultural officers ambao wameshindwa kupambana na wadudu hawa. Hili jambo haliko Kirinyaga pekee, wakulima wa Kisumu pia wanapitia changamoto hizi. Ni lazima tuwe na mazungumzo kuhusu vile Serikali itasaidia wakulima. Ajenda ya kwanza ya Serikali ya Kenya Kwanza ni kilimo, halafu afya, ujenzi wa barabara na elimu. Haya masuala yote iletwe pamoja. Kaunti ya Embu kuna chai, kahawa na maembe. Maembe pia imevamiwa na wadudu. Wakulima wanavuna maembe iliyo na ubora wa chini. Kilimo ni muhimu na Serikali inafaa iangalie masuala haya katika kaunti zote 47. Mimi ni Seneta wa Kaunti ya Embu. Wakulima wa Mbeere South na North wanapanda muguka. Mmea huu uko katika Crop Act. Kilimo cha muguka hakijaangaliwa vizuri. Wizara ya kilimo na Mifugo ya Hazina ya Jamhuri ya Kenya haijaangalia mazao ya kilimo ya muguka ili wakulima wanufaike. Serikali inafaa iwaajiri wasomi wa kilimo ili waangalie changamoto za wakulima katika kaunti zetu zote. Kaunti zote nchini zijengewe mabwawa za kunyunyuzia mazao ya wakulima maji. Pia Serikali ijenge water pans na boreholes. Mvua itanyesha hivi karibuni na hakuna hifadhi ya maji. Katiba ya Kenya imeashiria kuwa kilimo kimegatuliwa. Naomba Maseneta wakati wa bajeti tutenge pesa za kusaidia wakulima wakati mimea imepata magonjwa. Kampuni za mbegu zinawapatia wakulima mbegu mbaya, hasa za mahindi na maharagwe. Lazima tujiandae kama Seneti ili tuweze kusaidia wakulima wapate soko ya mazao yao nchi za nje. Hivi majuzi Serikali ilipendekeza chanjo kwa ng’ombe na mbuzi ili watu wa North Eastern wauze nyama ng’ambo. Chanjo siyo mbaya, lakini hakukuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}