GET /api/v0.1/hansard/entries/1525598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1525598,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525598/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ". Mmea wowote unafaa kufanyiwa research ili tuone jinsi ya kusaidia kila Mkenya. Baada ya hayo yote kufanyika, Serikali inafaa kutusaidia kwa mambo ya mazao yetu. Tukiuza katika nchi za ng’ambo, tunafaa kufuata njia inayofaa. Mmea wa makadamia umekumbwa na matatizo mengi. Wakati tulipochaguliwa, makadamia ilikuwa inauzwa kwa shilingi thelathini kwa kilo. Tulipoketi kama Maseneta na maafisa husika, bei ilipanda hadi shilingi 130. Kutokana na hilo, miezi ijayo, huenda watu wengi wakaanza kupanda mmea wa makadamia ili kuuza mazao yake katika nchi za ng’ambo. Naomba kuwe na public participation ili watu waambiwe kwa nini mazao ya mmea huo hayatanunuliwa. Wakulima waache kulia kwa sababu kuna shida zinazokumba mmea wa makadamia, licha ya kuwa watu kutoka kaunti mbalimbali wanaupanda. Mimi kama Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Agriculture, Livestock and Fisheries, naunga mkono Hoja hii. Kwa kumalizia, Bi. Spika wa Muda, mbegu yoyote haifai kukaa kwa muda mrefu."
}