GET /api/v0.1/hansard/entries/1525657/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1525657,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525657/?format=api",
    "text_counter": 44,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Swali langu kwa Waziri ni kuhusu dada zetu na changamoto wanazozipata ughaibuni wanapofanya kazi. Je, kuna mikakati gani ya uendeshaji wa hazina ya fedha ya kuwasaidia wanapokuwa kule nje? Nina imani kuna juhudi na jitihada nyingi ambazo Wizara imesaidia kwa kuwafanyia ile DNA test . Lakini kuna changamoto ya kifedha wanapopata zile birth certificates ambazo wanapewa. Je, kama Wizara kuna mikakati gani imewekwa kuona kwamba hazina hii inafanya kazi na kuwasaidia hawa dada zetu kule ughaibuni? Asante."
}