GET /api/v0.1/hansard/entries/1525696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1525696,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525696/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "sasa huyo mama ni mgonjwa sana. Ana presha na magonjwa tofauti tofauti yanayolazimu aidha apelekwe hospitali na akipona aweze kurudi nyumbani. Mama huyo anatoka Baraka Chembe huko eneo la Kaunti ya Kilifi. Kuna agency inaitwa Lahaza Agency iliyompeleka huko. Sasa akiwa na haja ya kuwafikia wale agents wake hawezi. Ni mgonjwa sana na kuna hatari anaweza kufariki. Bw. Waziri, je, unaelewa kwamba huyu mama yuko hali mahututi na hivi sasa anatakikana kurudi nyumbani? Hilo ndilo swali la kwanza. Swali la pili, je, hii Lalazar ama Hahazar Agency inaruhusiwa na Wizara yako kupeleka Wakenya kule Saudi Arabia kufanya kazi? Niko na jina la agent ambaye alihusika na kumchukuwa huyu mama kutoka Kilifi akampelela Saudia. Anaitwa Bw. Mohammed. Namba yake ya simu ni 0759297229. Je, huyu mtu anaruhusiwa kufanya hiyo kazi ya kupeleka watu Uarabuni? Huyu mama sasa hivi hawezi kufanya kazi yoyote ya nyumba ama ya uuguzi. Wewe kama Waziri na Wizara yako, unachukua hatua gani kuweza kumleta huyu mama nyumbani? Vile vile umechukua hatua gani kuona ya kwamba hii kampuni ambayo ilimpeleka imewajibika kuweza kumleta huyu mama nyumbani? Asante, Bw. Spika."
}