GET /api/v0.1/hansard/entries/1525698/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1525698,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525698/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Alfred Mutua",
"speaker_title": "The Cabinet Secretary for Labour and Social Protection",
"speaker": null,
"content": " Thank you, Mr. Speaker, Sir. Nitaanza na swali la Sen. Miraj kuhusu ile hazina ya fedha. Tayari tumepanga mikakati ya kuwa na hazina ya fedha ambayo itaondoa changamoto nyingi. Hivi sasa lazima hiyo hazina ya fedha iwe imeorodheshwa kwenye sheria. Kwa hivyo, tuko Mswada wa Labour Migration, ambao tayari niliweka sahihi juzi ndiyo iweze kuletwa kwa Bunge na iweze kuchangiwa ndiyo uwe sheria. Kwa hivyo, tunatarajia kwamba itakuja mpaka hapa na tutaweza kusonga nayo. The second question is from Sen. Mungatana. Thank you very much as that is a brilliant question. Kwa sababu Nairobi na Mombasa sio Kenya na miji mikuu sio Kenya, ni lazima tuwe na mikakati ya kuweza kuwafikia watu. Nilikuwa nimeaanza safari ya kuenda katika kila kaunti kuzungumza na ndugu na dada zetu lakini tukawa na upungufu wa hali ya fedha. Unajua kuna upungufu wa fedha kwa sababu bajeti yetu ilikatwa. Pia kulikuwa na changamoto kidogo ya zile safari nilienda. Niliona kuna agencies na mikakati ambayo kweli lazima kwanza yalainishwe ndio tusiende tukajichimbia shimo. Kwa hivyo, hayo ni mambo ambayo naendelea kumaliza na hivi karibuni nitarejea. Nataka kufanya kazi sana na waheshimiwa wa Seneti na wa Bunge la Kitaifa, ndiyo tuweze kushirikiana. Wakati naja mahali nawaeleza, mnapanga watu wenu na pengine hata mnawasaidia na nauli kidogo na tunaenda mahali ambapo ni karibu. Nikienda kaunti fulani, nisiende tu mahali pamoja niende recruitment kaunti nzima. Kuna mpango ambao naangalia ambapo nitaweza kuwauliza nyinyi wenyewe mkiwa kule kijijini muweze kuwatambua wale ambao wamehitimu, ndiyo tuanzie hapo. Isikuwe ni kazi yetu tu kuja hapo. Nyinyi ni waheshimiwa ambao mmepigiwa kura na wananchi. Mnastahili kuwawakilisha na kuwasaidia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}