GET /api/v0.1/hansard/entries/1525757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1525757,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525757/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa kwa mara ya pili. Ningependa kujua kama Bw. Waziri ana takwimu za watoto wanaorandaranda mitaani ambao wameongezeka. Wamekuwa watu wazima sasa na wanazaa watoto wengine ambao pia wanarandaranda kule Mjini Mombasa. Familia hizo sasa zimeanza kuishi katika sehemu za makaburi ikiwemo Mbaraki Cemetary na kufanya kuwa makazi yao. Ningependa Bw. Waziri atueleze mikakati iliyowekwa ili kutambua watoto wanaorandaranda ama kuna kipimo gani cha Serikali kinachoweza kujua jamii zinazorandaranda wakiwemo watoto hao na familia zao? Suala la watoto hao wanaorandaranda mitaani limeleta suitofahamu kwa sababu limechangia kuongezeka kwa utovu wa usalama katika maeneo mengine kule Mombasa. Je, ni mikakati gani iliyowekwa kutambua watoto wanaorandaranda na ni sababu gani wanaishi kule Mjini Mombasa? Vidole vya lawama vimekuwa vikielekezwa kwa Gavana anapojaribu kushughulikia suala la watoto hao. Je, ni hatua gani ambazo zimechukuliwa kuwatambua watoto wanaorandaranda na kwa nini wameongezeka kwa asimilia 80 katika Mji wa Mombasa?"
}