GET /api/v0.1/hansard/entries/1525760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1525760,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525760/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Cabinet Secretary for Labour and Social Protection",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kuokoa watoto, vijana na akina mama ambao huishi kwenye barabara ni jambo ambalo tumekuwa tukiangazia. Hatutangoja hadi wakati ambao tutafanya hesabu yao. Ni mpango ambao unaendelea ambao nimetilia mkazo. Wiki hii nilikuwa na mkutano kujadili mambo hayo kwa sababu yananikera. Sipendi kuona Wekenya wakihangaika barabarani ilhali nchi yetu ni huru. Lazima tuwapange ili warudi nyumbani na kuendelea na maisha ya heshima. Asante sana, Bw. Spika."
}