GET /api/v0.1/hansard/entries/1525822/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1525822,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1525822/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Hon. Mbadi ametueleza kuwa alipata ujumbe kutoka kwa Attorney-General (AG) ya kwamba jambo hili halifai kufanywa. Wakati Mhe. (Prof.) Ndung’u alihudhuria mkutano wa kamati hii, hakuwa amezungumza na AG kumweleza kuwa anakwenda kule na anataka kupewa ushawishi kabla ya kupeleka mkataba huu kwenye baraza la mawaziri. Walieleza kuwa ni lazima wangekuwa Cabinet Secretaries watatu ambao watapeleka joint Cabinet Memo ili pesa hizo ziwekwe kwenye bajeti. Ni lini swala hili lilibadilika? Ama huu ni mchezo wa paka na panya? Leo tunasema tunampa huyu lakini kwa sababu hana ile political clout wanatupwa nje. Maisha ya waliokuwa madiwani ni ya hofu. Ni lazima uwapiganie. Leo hii Hon. Mbadi akisema tunabadilisha na kuweka programu kama ya Inua Jamii itakuwa ni ubaguzi. Unaezaje kusema unainua jamii ya madiwani na kuwapa Kshs200,000 ilhali unmpa baba ya Ledama Kshs200? Je, huu ni ungwana? Asante."
}