GET /api/v0.1/hansard/entries/1526616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1526616,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1526616/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Bw. Spika, nadhani Waziri anaweza kujibu swali langu kwa sababu ni jambo ambalo limekuwa likisumbua watu wengi. Mnamo tarehe moja mwaka wa 2023, WRA iliongeza bei ya maji kwa wakulima na watu wengine. Mwezi wa saba mwaka wa 2023, kulikuwa na agizo la mahakama ambalo lilisimamisha watu ambao wanatumia maji kufanya ukulima na kunywa kulipishwa kodi mpaka kesi itakaposikilizwa. Je, kwa nini mpaka sasa hivi wananchi wa Kenya wanaendelea kulipishwa maji ambapo bei iliongezwa kutoka thumuni hadi shilingi tano kwa kila lita elfu moja ilhali kuna agizo la mahakama?"
}