GET /api/v0.1/hansard/entries/1526697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1526697,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1526697/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Mwaka jana, malumbano kama hayo yaliwacha wakulima majani chai kuchelewa kuleta mbolea. Kwa hivyo, ningetaka kujua, unafanya nini kumaliza malumbano yaliyoko katika taasisi ya KTDA. Swali langu la pili na la mwisho kuhusu macadamia. Nimeisoma tafsida yako uliyoileta siku ya leo. Kuna mahali ambapo hatutakubaliana nayo. Ninasema hivyo kwa sababu- Mwanzo, hii sheria iliyoletwa na AFA mwaka wa 2013 na ninamwona Mkurungenzi Mkuu wa AFA, Bruno Nyiru, yuko hapa. Kila mara tukiongea mambo ya makadamia, huwa najihisi kama tumealika mbu katika kongamano la kutafuta dawa za malaria. Walioleta sheria gandamizi katika Bunge la Kitaifa ni AFA. Na ndio maana hii sheria inaitwa AFA. Bw. Waziri, inakuwaje mkulima wa mahindi hashurutishwi na Serikali kwamba ili auze unga, lazima asiage mahindi? Inakuwaje mkulima wa kahawa anapopeleka kahawa sokoni yeye haambiwi aende akaushe, apike ile kahawa? Mpaka saa hii ukienda Bandari ya Lamu, wafugaji bado wanaruhusiwa kuuza ng’ombe wakiwa hai na bado tunahitaji ngozi. Iweje wakulima wa makadamia, korosho, Bixa, na wa pareto ndio waliwekewa sheria hususan ya kuwafinya? Mimi ni mkulima. Nimemsikia Bw. Waziri akisema ulikuwa na kikao na wakulima. Niliopa picha za watu wakiwa na makoti marefu na wengine wasio na nywele. Kama kuna mtu aliye mkulima wa makadamia ni mimi. Ninapoongea siku ya leo, naongea kwa niaba ya mkulima wa makadamia Tongaren ambaye hawezi kufika kwa kikao hiki akajieleza, mkulima wa Trans Nzoia anayeumia kwa sababu ya makadamia, mkulima wa Nyeri ambako umetoka, waliokutunuku nafasi kukaa katika Seneti yetu tukufu. Lakini ningependa kukuambia ya kwamba siku ya leo wanaumia. Mliokaa nao si wakulima. Jambo la pili ukipenda unaweza nitafuta ili nikupeleke kwa maghala. Hii ni kwa sababu soko ni mbili. Soko ya nchini na wale ambao wanaongeza thamana katika makadamia."
}